Pata taarifa kuu
NIGERIA-SIASA-RUSHWA-USALAMA

Bunge la Nigeria latishia kumtimua madarakani Buhari

Wabunge wa Nigeria wametishia kutumia utaratibu wa kumtimua madarakani Rais Muhammadu Buhari ikiwa hatua kali hazitachukuliwa kukabiliana na rushwa na kurejesha usalama nchini. Hali hiyo inaonyesha hali ya kutoelewana kati ya serikali na Bunge nchini Nigeria.

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari.
Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari. REUTERS /Stringer
Matangazo ya kibiashara

Bunge la Seneti na Baraza la wawakilishi wamesema katika azimio kwamba Bunge la taifa "halitosita (kutumia) mamlaka yake ya kikatiba kama hakuna kitakachofanyika". Azimio hilo lilitolewa baada ya "kikao cha pamoja" kilichochofanyika katika kikao cha faragha mjini Abuja.

Ofisi ya rais haijazungumzia chochote kuhusu azimio hilo lililotolewa na idara ya mawasiliano ya Rais wa Seneti Bukola Saraki, mwanachama wa All Progressive Congress (APC), chama madarakani.

Hata hivyo, kundi la wabunge wa chama cha APC walilaani katika taarifa siku ya Jumatano wiki hii azimio lililopitishwa "bila kura", baada ya mkutano uliohudhuriwa na wabunge wa upinzani.

Bw Buhari ambaye alichaguliwa mnamo mwaka 2015 kutokana na ahadi zake za kulitokomeza kundi la waasi la Boko Haram na kupambana dhidi ya rushwa, anaona kuwa utawala wake umeanza kukosolewa wakati anatarajia kuwania tena katika uchaguzi wa urais mwaka ujao.

Wapiganaji wa kijihadi, ingawa wamekua dhaifu, wanaendelea kufanya mashambulizi mabaya kaskazini-mashariki mwa Nigeria, wakati ambapo mapigano kati ya wakulima na wafugaji yanaendelea kuyakabili majimbo ya kati tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.