Pata taarifa kuu
SENEGAL-HAKI

Senegal: Kesi ya Khalifa Sall yaanza kusikilizwa katika Mahakama ya Rufaa

Nchini Senegal, miezi miwili baada ya kuhukumiwa miaka mitano jela, kesi ya meya wa Dakar, Khalifa Sall, inatarajiwa kuanza kusikilizwa Jumanne wiki hii katika Mahakama ya Rufaa.

Bango lenye maandishi "Khalifa Sall aachiliwe huru" (Julai 2017), picha ya kumbukumbu.
Bango lenye maandishi "Khalifa Sall aachiliwe huru" (Julai 2017), picha ya kumbukumbu. SEYLLOU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Upande wa Mashitaka na upande wa utetezi, wote walikata rufaa: Meya wa Dakar, ambaye anazuiliwa jela tangu mwezi Machi 2017, alipatikana na hatia ya udanganyifu na sio ubadhirifu wa fedha za umma.

Serikali, ambayo ilikua ikidai kutendewa haki kwa kulipwa fedha zote zilizoibwa na fidia pia, ilikataa rufaa dhidi ya hukumu ya miaka mitano aliyopewa Khalifa Sall. Ofisi ya mashitaka inaona kwamba adhabu hiyo haitoshi.

Kesi hii inaanza kusikilizwa katika Mahakama ya Rufaa na haijajulikana kama adhabu hiyo itaongezwa au kupunguzwa.

Wanasheria wa Khalifa Sall wanasema mteja wao hana hatia.

Kwa upande wa wanasheria wa serikali ya Senegal, wanasema kesi hii katika Mahakama ya Rufaa ni muhimu. Kwa sababu serikali ilifanyiwa unyonge katika mahakama ya mwanzo na imeomba kulipwa fedha zilizoibwa.

Ikiwa imesalia miezi minne tu kabla ya uchaguzi wa urais, ambapo Khalifa Sall anaweza kuwania katika uchaguzi huo, bado kesi yake inaendelea kuibua sintofahamu kwa wanasiasa nchini Senegal.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.