rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Niger Ufaransa Mahamdou Issoufou

Imechapishwa • Imehaririwa

Rais wa Nigeria Mahamadou Issoufou azuru Ufaransa

media
Mahamadou Issoufou (picha) atakutana na mtu na mwenyeji wake wa Ufaransa Emmanuel Macron, vyanzo vilivyo karibu na ofisi ya rais wa Niger vimesema ISSOUF SANOGO / AFP

Rais wa Niger Mahamadou Issoufou anatazamia kufanya ziara ya kiserikali nchini Ufaransa Jumatatu hii (Juni 4). Atapokea alasiri katika ikulu ya Elysee na mwenyeji wake Rais Macron. Ziara hii ya ushirikiano wa nchi mbili ambapo mazungumzo kai ya wawili hawa yatagubikwa na masuala ya usalama.


Hii ni ziara rasmi wakati ambapo Niger inaendelea kukumbwa na mdororo wa kifedha. Mikataba mitano ya Euro milioni Hamsini, sawa na Faranga CFA bilioni 33, itasainiwa kati ya Niger na taasi ya maendeleo ya Ufaransa "Alliance Francaise de developpement."

Fedha hizi zitasaidia katika upanuzi wa mtandao wa usambazaji wa umeme katika maeneo ya mijini na maendeleo ya huduma ya umeme katika maeneo ya vijijini, pamoja na mradi wa mseto huko Agadez wenye thamani ya karibu Faranga za CFA bilioni ishirini bilioni.

Kwa mujibu wa vyanzo vilivyo karibu na ofisi ya rais wa Nigeria, Rais Mahamadou Issoufou atakutana na mwenyeji wake wa Ufaransa, Emmanuel Macron, kabla kufanya mkutano wa pamoja na na wanahabari.

Rais Mahamadou Issoufou pia atkutana na Rais wa baraza la Seneti Gerard Larcher katika kujadili fedha za ziada katika utekelezaji wa wa mpango wake wa maendeleo ta kiuchumi na kijamii (PDES).