rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Ufaransa DRC

Imechapishwa • Imehaririwa

Koffi Olomide kukamatwa kwa madai ya unyanyasaji wa kingono

media
Mwanamuziki wa Rhumba Koffi Olomidé,mnamo mwezi April mwaka 2005. Seyllou / AFP

Mahakama nchini Ufaransa imetoa hati ya kukamatwa kwa Mfalme wa muziki aina ya Rumba raia wa DRC Koffi Olomide ambaye anadaiwa kushambulia kingono na kuwapiga wachezaji wake wanne wakiwa Paris kati ya mwaka 2002 na 2006.


Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 61 aliondolewa nchini Ufaransa mwishoni mwa mwezi Januari kufuatia madai ya unyanyasaji aliyotekeleza nchini Ufaransa.

Wachezaji wake wanne wameeleza kuwa walilazimishwa kufanya ngono mara kadhaa wakiwa Drc au ziarani huku wakitaja walipokuwa ufaransa walifungiwa chumbani kwa saa 24 chini ya ulinzi wa wanaume watatu katika kitongoji kimoja jijini Paris.

Wachezaji hao wameeleza mara kadhaa kulazimishwa kufanya ngono bila kutumia kinga hotelini lakini pia studio ambapo walipigwa pale walipokataa.

Kwa mujibu wa walalamika wamedai kufanya matakwa ya mwanamuziki huyo baada ya kutishiwa kukosa kibarua,madai ambayo yanadaiwa kusemwa na wachezaji wake wote wakike.