Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Wanaharakati 16 wazuiliwa DRC

Wanaharakati 16 wa kutetea haki za binadamu waliokuwa wanaadamana Alhamisi wiki hii Mashariki mwa DRC kulalamikia ukosefu wa usalama ikiwa ni pamoja na utekaji nyara, wamekamatwa.

Polisi yasambaratisha maandamano ya wanaharakati wa haki za binadamu DRC.
Polisi yasambaratisha maandamano ya wanaharakati wa haki za binadamu DRC. KUDRA MALIRO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kuanzia Ijumaa iliyopita, raia zaidi ya 20 wametekwa na watu wanaotaka kulipwa.

Maandamano hayo yalikuwa yanafanyika mjini Rutshuru katika jimbo katika jimbo la Kivu Kaskazini, wakati Polisi walipowakamata muda mfupi baada ya kuanza harakati hizo.

Polisi wanasema wanaharakati hao hawakuwa na kibali cha kuandamana.

Hayo yanajiri wakati ambapo mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, Bi Leïla Zerugwi amesema Monusco inaendelea kuhakikisha kuwa Uchaguzi Mkuu unafanyika nchini humo mwezi Desemba mwaka huu.

Aidha amesema, katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres anasubiriwa nchini DRC mwezi ujao, wakati huu serikali ya nchi hiyo ikilitaka jeshi la MONUSCO kuondokaifikapo mwaka 2020.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.