Pata taarifa kuu
NIGERIA-SIASA

Vijana wapewa nafasi kuwania nyadhifa mbalimbali za kisiasa Nigeria

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, ametia saini kuwa sheria mswada unaopunguza umri kwa wananchi wa taifa hilo wanaotaka kuwania nyadhifa mbalimbali za kisiasa.

Rais Muhammadu akisaini sheria inayopunguza umri kwa wananchi wa Nigeria wanaotaka kuwania nyadhifa mbalimbali za kisiasa.
Rais Muhammadu akisaini sheria inayopunguza umri kwa wananchi wa Nigeria wanaotaka kuwania nyadhifa mbalimbali za kisiasa. RFI/Kabir Yusuf
Matangazo ya kibiashara

Sasa ni rasmi kuwa, raia wa Nigeria mwenye umri wa miaka 35 anaweza kuwania urais kuanzia Uchaguzi Mkuu wa mwaka ujao, umri wa chini ulikuwa miaka40.

Wanaotaka kuwania ubunge, wanastahili kuwa na umri wa miaka 25 na kuendelea huku wale wanotaka kuwa Maseneta na Magawavana wanastahili kuwa na umri wa miaka 35.

Rais Buhari mwenye umri wa miaka 75, tayari amesema atatetea kiti chake kwa muhula wa pili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.