rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Joseph Kabila

Imechapishwa • Imehaririwa

Upinzani waendelea kupinga matumizi ya mashine zakupigia kura DRC

media
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Corneille Nangaa, Novemba 5, 2017, Kinshasa. JOHN WESSELS / AFP

Upinzani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo umesema hawatakubali tume ya Uchaguzi CENI kutumia mashine za kielekroniki wakati wa uchaguzi mkuu unaopangwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu


Haya yanajiri wakati mmoja wa wanasiasa hao wa upinzani, Martin Fayulu, pia ametangaza nia yake ya kugombea kiti cha urais wakati wa uchaguzi huo.

Bw Fayulu amesema kuwa kuna haja ya kufanyika mabadiliko katika mfumo wa kisiasa wa nchi hiyo, na kwamba hawataki rais Joseph Kabila aongoze kipindi cha mpito.

Katika hatua nyingine Tume ya Uchaguzi CENI imesema inaendelea vizuri na maandalizi ya uchaguzi huo, maandalizi ambayo upinzani unasema yanatia hofu ya kuwa na uchaguzi huru, haki na wakuaminika.

Nacho chama tawala cha PPRD kimeendelea kumwandalia rais Kabila mazingira ya kuwania muhula wa tatu. Hali ambayo huenda ikazusha vurugu nchini humo.