Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-SIASA

Uchaguzi mkuu kufanyika Julai 30 Zimbabwe

Uchaguzi wa kwanza wa urais na wa ubunge baada ya Robert Mugabe utafanyika Julai 30 nchini Zimbabwe. Mrithi wake na msaidizi wake wa zamani, Emmerson Mnangagwa, anapewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo wa urais.

Rais Emmerson Mnangagwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chama cha Zanu-PF kwa uchaguzi mkuu wa Julai 2018 huko Harare, Mei 4, 2018.
Rais Emmerson Mnangagwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chama cha Zanu-PF kwa uchaguzi mkuu wa Julai 2018 huko Harare, Mei 4, 2018. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni Bw Mnangagwa alitangaza kwamba " siku ya Jumatatu Julai 30, 2018 itakuwa ni siku ya uchaguzi wa uais, uchaguzi wa ubunge na uchaguzi wa madiwani," gazeti la serikali limetangaza Jumatano wiki hii.

Duru ya pili ya uchaguzi wa urais imepangwa kufanyika Septemba 8. Duru hii itafanyika kama hakutakua na mgombea ambaye atakua amepata zaidi ya asilimia hamsini ya kura katika duru ya kwanza.

Aliyekuwa Makamu wa rais, Emmerson Mnangagwa, mwenye umri wa miaka 75, alifaulu kumrithi mano mwezi Novemba mwaka jana, mtangulizi wake Robert Mugabe, mwenye umri wa miaka 94, ambaye alilazimika kuashia madaraka kufuatia shinikizo la jeshi na chama chake tawala, baada ya kutawala bila kugawana madaraka tangu uhuru wa nchi hiyo mwaka 1980.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.