Pata taarifa kuu
SOMALILAND-PUNTLAND-RSF-VYOMBO VYA HABARI

RSF yalaani kukamatwa kwa wanahabari Somaliland

Shirika la kimataifa linalotetea Haki za waandishi wa Habari (RSF) limeshtumu vikali kukamatwa kwa waandishi wa habari na kufungwa kwa vituo viwili binafsi vya televisheni huko Somaliland.

Mwandishi wa habari wa SBS Mohamed Ahmed Jama Bidhanshe na Abdirahman Keyse Tungub, mwandishi wa habari wa Bulsho TV.
Mwandishi wa habari wa SBS Mohamed Ahmed Jama Bidhanshe na Abdirahman Keyse Tungub, mwandishi wa habari wa Bulsho TV. Twitter/RSF
Matangazo ya kibiashara

Serikali inashtumu waandishi hao wa habari na vituo hivyo vya televisheni kurusha hewani taarifa kuhusu maandamano ya hivi karibuni na makabiliano kwenye mpaka Kusini-Mashariki mwa taifa hilo lililojitangazia uhuru katika Pembe Afrika.

"RSF inaomba serikali ya Somaliland kusitisha mara moja ukandamizaji unaoendelea dhidi ya vyombo vya habari binafsi," RSF imesema katika taarifa yake.

Chama cha waandishi wa habari nchini Somalia (NUSOJ) kimeelezea kuguswa na unanyasaji huo dhidi ya waandishi wa habari wa vyombo vya habari binafsi.

Mamlaka inashtumu waandishi wa habari na vyombo vya habari kurusha hewani taarifa kuhusu mgogoro kati ya majeshi ya somaliland na yale ya eneo linalojitawala la Puntland (kaskazini mwa Somalia) katika eneo la jangwa linalodaiwa na pande zote mbili na ambalo linapatikana kati ya miji ya Las Anod (Somaliland) na Garowe (Puntland).

Kwa mujibu wa RSF, serikali ya Somaliland imeamua kufunga matangazo ya vituo vya televisheni binafsi, SBS na SOMNews, ikivishtumu "kushiriki katika kampeni za kisiasa" kwa kurusha hewani taarifa kuhusu maandamano ya hivi karibuni dhidi ya Somaliland huko Las Anod.

RSF pia inalaani kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni SBS Mohamed Ahmed Jama Bidhanshe siku ya Jumatatu alipokua akiendesha kazi yake kuhusu maandamano hayo na mwanahabari wa kituo cha televisheni Bulsho TV, Abdirahman Keyse Tungub, aliyetoa taarifa kuhusu wakazi wa eneo hilo kukata tamaa kufuatia kuzuka kwa mapigano kati ya Puntland na Somaliland.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.