Umoja wa Mataifa waadhimisha siku ya kimataifa ya walinda amani
Umoja wa Mataifa hivi leo unatimiza miaka 70, tangu ulipoanza kutuma wanajeshi wake wa kulinda amani kusaidia kurejesha amani katika mataifa mbalimbali ya dunia.
Imechapishwa:
Ni siku ya kuwakumbuka wanajeshi wa kulinda amani 3,700 ambao tangu mwaka 1948, huku walinda amani 129 wakipoteza maisha mwaka uliopita.
Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inasalia nchi yenye idadi kubwa ya wanajeshi wa kulinda amani zaidi ya elfu 15, 000 kusaidia kulinda amani hasa Mashariki mwa nchi hiyo.
Umoja wa Mataifa ulianzishwa Oktoba 24, 1945 huko San Francisco nchini Marekani.
Siku hiyo mataifa 50 yalitia saini makubaliano ya kuanzisha chombo hicho kilichokuwa na lengo na kulinda Amani na usalama, kuendeleza ushirikiano baina ya mataifa kwa lengo la kujikwamua kiuchumi na kijamii na kulinda haki za binadamu.