rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Ebola Afya

Imechapishwa • Imehaririwa

Ebola yaendelea kuathiri raia DRC

media
Mwuguzi wa WHO akionyesha kifuko ambapo ndani yake kuna chanjo ya Ebola, Mbandaka, DRC, Mei 21, 2018. JUNIOR KANNAH / AFP

Mchungaji mmoja wa Kanisa katoliki amewekwa kwenye uangalizi maalumu baada ya kupata maambukizi ya virusi hatari vya ugonjwa wa Ebola kwenye mji wa Mbandaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.


Kwa mujibu wa maofisa wa afya wanasema mchungaji huyo alipata maambukizi baada ya kumuombea mgonjwa aliyekuwa na viruso hivyo, tukio linalojiri wakati huu kampeni ya utosaji chanjo ikiendelea.

Dokta Toure Al Hassan mtaalamu wa magonjwa mlipuko kutoka Guinea, anasema ni lazima jamii ielimishwe na kuhamasishwa kuhusu hatari ya virusi hivi na umuhimu wa kupatiwa matibabu.

Mpaka sasa kunaripoti kuwa watu zaidi ya 30 wameshapoteza maisha kutokana na virusi vya ugonjwa wa Ebola huku shirika la afya duniani WHO likionya kuhusu uwezekano wa kuenea kwa maambukizi zaidi.