rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Joseph Kabila

Imechapishwa • Imehaririwa

Mabango yenye picha ya Kabila yazua sintofahamu DRC

media
Mpaka sasa Rais Joseph Kabila hajazungumzia nia yake ya kuwania au la katika uchaguzi huo. REUTERS/Kenny Katombe

Mabango yenye picha ya rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, yakiwa na maandishi kuwa Kabila ni "mgombea" wa kiti cha urais katika uchaguzi wa Desemba 23 yamezua hali ya hasira miongoni mwa wanasiasa wa upinzani na mashirika ya kiraia nchini humo.


Mabango hayo yaliyobuniwa na wafuasi wa chama tawala cha PPRD yameonekana katika maeneo ya umma, kama vile Soko la Lalu, katika wilaya ya Binza Delvaux, magharibi mwa jiji kuu Kinshasa.

Wadadisi wa mambo wanaona kuwa mpango huo ulioanzishwa na chama hicho ni ā€œmkakati hatari" kwa mchakato wa uchaguzi nchini humo.

Uchaguzi mkuu nchini DRC umepangwa kufanyika Mnamo mwezi Desemba mwaka huu.

Lakini wanasiasa nchini DRC hawajaafikiana kama kweli uchaguzi huo utafanyika Rais Kabila akiwania kwa muhula mwingine.

Jambo hilo limekua likizua sintofahamu, lakini mpaka sasa Rais Joseph Kabila hajazungumzia nia yake ya kuwania au la katika uchaguzi huo.