Pata taarifa kuu
DRC-HWO-EBOLA-AFYA

Vifo kutokana na mlipuko wa Ebola vyaongezeka DRC

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na Ebola, imeongezeka wakati chanjo dhidi ya ugonjwa huo ilianza kutolewa Jumatatu wiki hii. Vifo vilivyosababishwa na ugonjwa wa Ebola vimeongezeka mpaka kufikia 27.

Mwuguzi wa WHO akionyesha kifuko ambapo ndani yake kuna chanjo ya Ebola, Mbandaka, DRC, Mei 21, 2018.
Mwuguzi wa WHO akionyesha kifuko ambapo ndani yake kuna chanjo ya Ebola, Mbandaka, DRC, Mei 21, 2018. JUNIOR KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema limewatambua zaidi ya watu 500 ambao huenda wamekaribiana na waathiriwa wa ugonjwa wa Ebola nchini Congo.

Vifo vilivyosababishwa na ugonjwa wa Ebola vimeongezeka mpaka kufikia 27.

Maafisa wa shirika la Afya Duniani (WHO) na Serikali ya Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo walianzisha mpango wa kutoa chanjo ya majaribio dhidi ya ugonjwa wa Ebola ili kudhibiti kusambaa zaidi kwa virusi vya ugonjwa huo.

Awamu ya kwanza ya chanjo hiyo ya majaribio iliwasili nchini Congo siku ya Jumatano.

Kumekuwa na milipuko mitatu ya Ebola nchini DRC tangu janga la mwaka 2014-2016 katika Afrika ya magharibi.

Kampeni rasmi ya kutoa chanjo ya kudhibiti maambukizi ya virusi hatari vya ugonjwa wa Ebola imeanza, wakati huu shirika la Afya duniani WHO likisema maambukizi ya DRC sio hatari kidunia kwa sasa.

Jumla ya dozi laki 3 za chanjo za ugonjwa huo zimeahidiwa kutolewa na nchi washirika wa DRC huku Shirika la Afya Duniani (WHO) likisema linafikiria pia kutumia chanjo iliyotengenezwa na kampuni nyingine ya Johnson and Johnson.

Mpaka sasa jumla ya watu 25 wamethibitishwa kupoteza maisha kaskazini magharibi mwa nchi ya DRC kwenye mji wa Bikoro huku watu zaidi ya 45 wakiripotiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huu.

Kumekuwa na hofu kuwa ugonjwa huu huenda ukafika kwenye jiji la Kinshasa kupitia mto Congo ambao unatenganisha jiji hilo na mji wa Mbandaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.