Pata taarifa kuu
MAREKANI-CAMEROON-USALAMA

Marekani yashutumu Cameroon kwa mauaji ya kuvizia

Marekani imeishutumu serikali ya Cameroon kwa "mauaji ya kuvizia" katika maeneo ya nchi hiyo wanakozungumza Kiingereza yanayoendelea kukumbwa na mgogoro wa kijamii na kisiasa.

Rais wa Cameroon Paul Biya.
Rais wa Cameroon Paul Biya. LUDOVIC MARIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Marekani pia imeshtumu wanaharakati wenye silaha wanaotaka kujitenga kwa maeneo yao kuhusika na "mauaji ya polisi" na "kuwateka nyara watumishi wa umma", kulingana na taarifa ya serikali ya Marekani iliyotolewa Ijuma wiki hii.

"Kwa upande wa serikali, kumekua na mauaji ya kuvizia, visa vya watu kuzuiliwa bila ya kupata msaada wa kisheria kwa familia au kwa Shirika la Msalaba Mwekundu, na uhasama (bila kusahau) uporaji katika vijiji mbailmbali" katika mikoa ya wanakozungumza Kiingereza na Kusini-Magharibi mwa nchi, taarifa ya Balozi wa Marekani nchini Cameroon imebaini.

Balozi wa Marekani nchini Cameroon, Peter Henry Barlerin, ambaye alikutana siku ya Alhamisi wiki hii na Rais wa Cameroon Paul Biya katika mji wa Yaounde, pia manashtumu wanaharakati wenye silaha wanaotaka kujitenga kuhusika na vifo vya "maafisa wa polisi na, utekaji nyara, na kuchoma moto shule ".

Katika maeneo ya kaskazini magharibi na kusini magharibi, vita vimekua vikitokea kila kukicha kati ya vikosi vya usalama vya Cameroon na watu wenye silaha kutoka jimbo kwanakozungumza Kiingerezazi, Jimbo hili lilianzishwa kati ya vita vya kwanza na vya pili vya dunia, chini ya mamlaka ya Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.