rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC

Imechapishwa • Imehaririwa

Mashirika ya kiraia yalaani vitendo vya utekaji nyara DRC

media
Msafara wa magari ukisubiri kusindikizwa na askari karibu na Hifadhi ya Taifa ya Wanyamapori ya Virunga, mashariki mwa DRC. RFI/Sonia Rolley

Muungano wa mashirika ya kiraia katika jimbo la Kivu ya Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamepinga kukithiri kwa vitendo vya utekaji nyara mashariki mwa nchi hiyo.


Siku ya Jumapili, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Boris Johnson alithibitisha kuachiliwa huru kwa watalii wawili wa Uingereza waliokuwa wametekwa nyara katika Hifadhi ya Wanyamapori ya Virunga, mwishoni mwa juma lililopita.

Hata hivyo hakuna taarifa zaidi kutoka kwa Waziri huyo kuhusu mazingira ya kuachwa huru wala wahusika wa Utekaji wa watalii hao.

Mashirika ya kiraia nchini DRC yamelaani vkitendo hicho cha utekaji nyara, na kusema kuwa ni maadui wa nchi hiyo ndio wametekeleza kitendo hicho kiovu.

Mashuhuda wanasema mlinzi mmoja wa mbuga hiyo aliuawa kwa kupigwa risasi, baada ya kuvamiwa na watu wenye silaha.