rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Togo Faure Gnassingbe

Imechapishwa • Imehaririwa

Upinzani wafuta maandamano yaliyokua yalipangwa wiki hii Togo

media
Wafuasi wa upinzani wanakusanyika wakati wa maandamano ya kumtaka rais Faure Gnassingbe kujiuzulu haraka,Lome, Togo, Septemba 7, 2017. REUTERS/ ...

Nchini Togo, upinzani unaoendelea na maandamano ya kupinga utawala wa rais Faure Gnassingbe kwa miezi saba sasa umetangaza kwamba umefuta maandamano yaliyokua yamepangwa wiki hii nchini humo.


Maandamano hayo yalipangwa kuanza Jumatano wiki hii katika mji mkuu wa nchi hiyo, Lome na katika miji mingne mikubwa.

Maandamano hayo hayatofanyika kwa muda wa siku mbili, kwa mujibu wa chanzo kutoka upinzani.

Serikali haikupiga marufuku maandamano hayo, lakini ilikua ilitoa barabara ambazo zingelitumiwa kwa maandamano hayo, hatua ambayo upinzani ulifutilia mbali.

"Muungano wa (vyama 14 vya upinzani) umeamua kusitisha kuandamana kwa siku mbili mfululizo kwa ombi la raia wa Togo," upinzani nchini Togo umesema katika taarifa yake.

Hata hivyo, upinzani umetoa wito kwa "wananchi wa Togo", nchini na wale waishio katika nchi za kigeni, kuwa makini na kuwa tayari kufuata maelekezo ya siku chache zijazo".