Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA

Libya: Marshal Haftar aanzisha operesheni kabambe dhidi ya Derna

Kundi linaloongozwa na Marshal Khalifa Haftar limezindua operesheni kabambe kwa minajili ya kudhibiti mji wa Derna, kilomita 1000 mashariki mwa mji mkuu wa Libya, Tripoli.

Marshal Haftar atangaza uzinduzi wa operesheni kabambe kwa minajili ya kuikomboa  Derna Mei 7, 2018, Benghazi.
Marshal Haftar atangaza uzinduzi wa operesheni kabambe kwa minajili ya kuikomboa Derna Mei 7, 2018, Benghazi. Abdullah DOMA / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Muda umewadi wa kuukomboa mji wa Derna", amesema Marshal Haftar.

Mji wa Derna uko chini ya udhibiti wa muungano wa wanamgambo wa Kiislamu na wanajihadi.

Kwa mujibu wa Marshal Haftar mashambulizi tayari yameanza dhidi ya "ngome za magaidi".

Derna inazingirwa kwa miezi kadhaa sasa. Marshal Haftar anadai kuwa amejaribu kujadili, lakini, kwa mujibu wa kiongozi huyo, juhudi hizi za amani zimegonga mwamba. Njia ambayo inatakiwa kutumia kwa sasa ni vita, ameongeza.

Miaka minne sasa imekamilika baada ya kuanzisha mashambulizi ya kuteka eneo la mashariki. Marshal Haftar amebaini kwamba mashambulizi yake dhidi ya makundi mbalimbali ya wanamgambo wanaodhibiti eneo hilo yatatekelezwa kwa neema ya kuweka mji wa mwisho ambao bado haujadhibitiwa na majeshi yake mashariki mwa Libya. Mji wa Derna bado uko mikononi mwa makundi yenye uhusiano na al-Qaeda kwa miaka mitatu.

Marshal Haftar ametangaza uzinduzi wa operesheni hiyo kabambe mbele ya majeshi yake. Maelfu ya askari wake walikusanyika Jumatatu wiki hii kwa gwaride la kijeshi mjini Benghazi, ambapo Marshal Haftar alihuduria.

Hivi karibu vyombo vya habari vya Libya vilitangaza kwamba hali ya afya ya Marshal Haftar iko hatarini, lakini washirika wake wa karibu walikanusha taarifa hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.