Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Jeshi lakomboa watu 1000 kutoka Boko Haram Nigeria

Nchini Nigeria majeshi yamefaulu kukomboa watu 1000 waliokua wakishikiliwa mateka na Boko Haram. Operesheni hiyo ilizinduliwa na majeshi kutoka nchi tano za ukanda wa Sahel pamoja na yale kutoka Chad na Cameroon.

Majeshi ya Nigeria katika operesheni kabambe dhidi ya Boko Haram.
Majeshi ya Nigeria katika operesheni kabambe dhidi ya Boko Haram. REUTERS/Tim Cocks
Matangazo ya kibiashara

Wengi wa mateka hao walikuwa wanawake na watoto, na vijana ambao walilazimishwa kupigana upande wa makundi ya wanamgambo wa Kiislamu, jeshi la Nigeria limesema.

Operesheni hiyo iliendeshwa katika vijiji vinne karibu na Bama, chanzo cha jeshi la Nigeria kimesema.

Boko Haram kwa karibu miaka kumi imeendelea na harakati zake mbaya kaskazini mashariki mwa Nigeria, ambako inataka kuweka taifa la Kiislamu.

Kundi hilo limedhoofika katika miaka ya hivi karibuni na limekataa kuweka chini silaha, lakini Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, madarakani tangu mwaka 2015, bado hajatekeleza ahadi yake ya kutokomeza vurugu katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.