rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Nigeria Boko Haram Muhammadu Buhari

Imechapishwa • Imehaririwa

Shambulio laua watu 45 kaskazini mwa Nigeria

media
Wapiganaji kadhaa waliendesha shambulizi dhidi ya jamii ya Birnin Gwari katika jimbo la Kaduna, Nigeria. Solacebase

Watu wasiopungua 45 waliuawa Jumamosi, mwishoni mwa juma hili na watu wasiojulikana katika kijiji cha Gwaska, katika jimbo la Kaduna, kaskazini mwa Nigeria, polisi imesema Jumatatu wiki hii.


"Tulipata miili 12 jana na 33 leo," Kamishna Austin Iwar ameliambia shirika la habari la Reuters.

Kijiji hiki, kinachopatikana katika eneo la Birnin-Gwari, kiko karibu na eneo la msitu linalojulikana kwa uhalifu.

Eneo la kaskazini mashariki la Nigeria bado linakabiliwa na mashambulizi ya kundi la Boko Haram, licha ya ahadi za Rais Muhammadu Buhari, ambaye aliahidi kutokomeza kundi hili. Rais Buhari ambye yuko madarakani tangu mwaka 2015, atawania muhala mwengine wa miaka minne mwaka ujao.