Pata taarifa kuu
MSUMBIJI-SIASA

Afonso Dhlakama, kiongozi wa upinzani Msumbiji afariki dunia

Kiongozi wa siku nyingi wa upinzani na waasi nchini Msumbiji Afonso Dhlakama, amefariki dunia. Alikuwa kiungo muhimu katika siasa za Msumbiji. Afonso Dhlakama, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, alifariki dunia Alhamisi, Mei 3 akiwa na umri wa miaka 65.

Kiongozi wa upinzani nchini Msumbiji, Afonso Dhlakama, hapa mwaka 2009, amefariki akiwa na umri wa miaka 65 Alhamisi, Mei 3, 2018.
Kiongozi wa upinzani nchini Msumbiji, Afonso Dhlakama, hapa mwaka 2009, amefariki akiwa na umri wa miaka 65 Alhamisi, Mei 3, 2018. REUTERS/Grant Lee Neuenburg
Matangazo ya kibiashara

 

Maafisa wa chama hicho wamesema mwanasiasa huyo wa upinzani wa muda mrefu alipatwa na mshtuko wa moyo uliosababisha kifo chake.

Kiongozi wa zamani wa waasi, Afonso Dhlakama aliongoza Renamo kwa miaka 39.

Harakati zake, Afonso Dhlakama, alizianza wakati wa uhuru. Alijiunga na Frelimo. Mwaka wa 1975, uhuru ulipatikana na mwaka mmoja baadaye, Afonso Dhlakama aliachana na chama hicho kiliokua na uhusiano wa karibu na Moscow kwa mujibu wa kiongozi huyo.

Kwa msaada wa utawala wa ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini, nchi jirani, Dhlakama alishiriki katika kuundwa kwa chama cha Renamo. Afonso Dhlakama aliongoza chama hiki mnamo mwaka 1979.

Hali ya kisiasa nchini Msumbiji ilidorora na nchi hii ilitumbukia katika miaka 16 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe hadi mwaka 1992, wakati Afondo Dhlakama alisaini makubaliano ya amani na rais wa zamani Joaquim Chissano.

Baada ya tarehe hiyo, Renamo iligeuka kuwa chama cha kisiasa cha jadi. Afonso Dhlakama akawa kiongozi wa upinzani na alishiriki katika uchaguzi zote za urais.

Lakini mwaka 2013, Renamo iliamua kuchukua tena silaha katikati mwa nchi hiyo. Chama hiki kilishtumu chama tawala kwa kuchukua udhibiti wa jimbo lao. Baada ya kukimbilia milimani Afonso Dhlakama hata hivyo alitangaza kusitisha mapigano ili kuendeleza mazungumzo na serikali. Ingawa hakuna mkataba rasmi ulisainiwa na serikali, makubaliano hayo yalizingatiwa na kuheshimiwa na pande zote mbili.

Hivi karibuni, alikutana na rais wa nchi hiyo Filipe Nyusi na wakakubaliana kuhubiri amani na mariadhiano baada ya miaka mingi ya mapigano, kama ilivyokuwa mwaka 2014 alipotia saini mkataba wa amani na rais wa zamani Armando Guebuza.

Katika miezi ya hivi karibuni, mazungumzo ya amani yalipelekea kuepo na mafanikio makubwa. Kifo chake kinaweza kuitumbukiza nchi hii hatarini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.