rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afrika Ulaya Amerika Vyombo vya Habari

Imechapishwa • Imehaririwa

Dunia yaadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya Habari

media
Uhuru wa vyombo vya habari umeshuka kwa karibu theluthi mbili duniani, kulingana na ripoti ya mwaka 2017 ya shirika la wanahabari la Reporters Without Borders (RSF). Reporters sans Frontières

Leo ni siku ya uhuru wa vyombo vya Habari duniani. Siku hii hutumiwa kuthathmini hali ya uhuru wa vyombo vya habari, kutoa taarifa katika mataifa mbalimbali duniani kwa uhuru, kupinga unyanyasaji wa wanahabari na kuwakumbuka wanahabari ambao wamepoteza maisha wakiwa katika maeneo ya kazi.


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress amewataka viongozi wa dunia kuheshimu uhuru wa vyombo vya Habari, suala ambalo bado linasalia changamoto hasa kwa mataifa ya Afrika.

Nchini Burundi wanahabari wanasema wanafanya kazi kwa uoga na katika mazingira magumu.

Wanahabari wengi waliuawa na wengine wamefungwa na wale ambao hawajakabiliwa na hali hiyo wanafanya kazi yao kwa uoga. Hali hii inashuhudiwa katika nchi ambazo zinaendelea kuminya uhuru wa habari, hasa barani Afrika na baadhi ya nchi za Asia na Amerika Kusini.