Pata taarifa kuu
SOMALIA-USALAMA-MAJANGA ASILI

Amisom waokoa watu 10,000 waliothiriwa na mafuruko Somalia

Wanajeshi wa Umoja wa Afrika nchini Somalia wamefanikiwa kuwaokoa raia wa nchi hiyo zaidi ya 10,000 waliothiriwa na mafuruko makubwa kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Askari wa Amisom wakipiga doria mbele ya Msikiti, Mogadishu, mji mkuu wa Somalia.
Askari wa Amisom wakipiga doria mbele ya Msikiti, Mogadishu, mji mkuu wa Somalia. REUTERS/Ismail Taxta
Matangazo ya kibiashara

Kamanda wa majeshi kutoka Djibouti Kanali Abdurahman Rayale Hared, ambayo yamehusika pakubwa kuwaokoa waathiriwa hao katikati ya nchi hiyo, amesema wataendelea kuwasaidia raia hao.

Mafuruko yamewaacha maelfu kukosa makaazi, chakula na dawa.

Hayo yanajiri wakati ambapo visa vya utekaji nyara vinaendelea kukithiri nchini humo. Mfanyakazi wa shirika la kimataifa la msalaba mwekundu, raia wa Ujerumani, ametekwa nyara katika mji mkuu wa Somalia.

Kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu, muuguzi huyo aliyetekwa alikuwa akifanya kazi kila siku kuokoa maisha ya baadhi ya Wasomali wenye hali mbaya.

Msemaji wa Shirika la Kimataifa la Msalaba mwekundu amesema wana wasiwasi mkubwa na usalama wa mfanyakazi mwenzao.

Serikali ya Somalia imesema inachunguza utekaji nyara wa muuguzi huyo ambaye amekuwa akitoa huduma za afya kwa raia wa nchi hiyo ambayo imeendelea kukabiliana na ugaidi kutika kundi la Al Shabab.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.