rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Nigeria Boko Haram Mauaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Watu zaidi ya 60 waangamia katika mashambulizi mawili Nigeria

media
Mubi, kaskazini mashariki mwa Nigeria. Wikipedia.

Watu zaidi ya 60 wameuawa katika jimbo la Adamawa, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria baada ya kutokea kwa mashambulizi mawili ya bomu yaliyolenga msikiti na soko.


Licha ya kuwa hakuna mtu au kundi ambalo limedai kuhusika na mashambulizi haya, mji wa Mubi katika jimbo la Adamawa kaskazini mashariki mwa Nigeria, umekua ukilengwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya Boko Haram. Mnamo mwezi Novemba mwaka uliyopita, watu 50 waliuawa katika mashambulizi ya awali.

Hata hivyo maafisa wa usalama wanasema mashambulizi hayo ya kujitoa mhanga, yalitekelezwa na wavulana wadogo waliotumwa na kundi la Boko Haram.

Watu wengine zaidi ya 60 walijeruhiwa baada ya mashambulizi hayo.

Awali msemaji wa jimbo hilo alibaini Jumanne mchana kwamba watu 27 waliuawa na karibu sitini walijeruhiwa katika mashambulizi hayo. Msemaji wa polisi wa eneo hilo anasema kuwa kwa uchache watu 24 waliuawa. Lakini kulingana na shirika la habari la AFP likinukuu mashahidi, watu wengi waliangamia katika mashambulizi hayo.

Mashambulizi haya ya kujitoa mhanga yalitokea mapema mchana. Mshambuliaji wa kwanza wa kujitoa mhanga alilipua mkanda wake uliokua umejaa vilipuzi katika moja ya misikiti ya mji huo wakati wa sala ya mchana. Dakika chache baadaye, wakati ambapo waumini walikua wakikimbia kutoka msikitini, mshambuliaji mwingine alijitokeza na kujilipua kwenye soko lililo karibu na msikiti huo.

Waathirika wote walipelekwa katika hospitali nne tofauti katika mji wa Mubi na maeneo jirani