rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

EAC Afrika Ulaya Amerika

Imechapishwa • Imehaririwa

Siku ya Kimataifa ya wafanyakazi yaadhimishwa

media
Kumekua na maandamano ya hapa na pale kufuatia madai ya wafanyakazi kuhusu mshahara wakisema mshahara wanaopewa haikidhi mahitaji yao ya kila siku. Hapa madakari wakiandamana huko Nairobi, Kenya le Februari 13, 2017. REUTERS/Thomas Mukoya

Wafanyakazi kote duniani, wanaadhimisha siku hii kwa kusherehekea mafanikio yao lakini pia kuangazia changamoto zinazowakumba katika maeneo ya kazi.


Viongozi wa vyama vya wafanyakazi hutumia siku kama ya leo kuwataka waajiri kuwaongezea wafanyakazi mshahara na kuboresha mazingira ya kufanya kazi.

Ni siku ambayo inaadhimishwa pia katika mataifa ya Afrika Mashariki na Kati.

Siku hii imefika wakati ambapo katika mataifa mengi kunashuhudiwa mfumuko wa bei za chakula, huku mshahara ukisalia pale pale.

Wafanyakazi katika sekta ya umma na ile binafsi wamekua wakilalamikia mishahara duni, huku wakiomba kuongezwa mishahara kutoka na hali ya maisha inayoendelea.

Baadhi ya serikali zimejitahidi kuongeza mshahara, lakini pia kuna zingine ambazo zimejitetea kuwa mshahara wanaolipwa wafanyakazi unatosha.

Kumekua na maandamano ya hapa na pale kufuatia madai ya wafanyakazi kuhusu mshahara wakisema mshahara wanaopewa haikidhi mahitaji yao ya kila siku.