Pata taarifa kuu
GABON-SIASA-HAKI

Bunge lavunjwa Gabon, serikali yachukuliwa vikwazo

Mahakama ya Katiba nchini Gabon imechukua uamuzi wa kuvunja Bunge na kuitaka serikali kujiuzulu kwa sababu imeshindwa kuandaa uchaguzi wa wabunge kwa wakati.

Mahakama ya Katiba ya Gabon wakati wa kuchukua uamuzi wake Libreville mwaka 2016 (picha ya kumbukumbu).
Mahakama ya Katiba ya Gabon wakati wa kuchukua uamuzi wake Libreville mwaka 2016 (picha ya kumbukumbu). STEVE JORDAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya Gabon ilipewa muda hadi mwisho wa mwezi Aprili kufanya hivyo, yaani hadi jana usiku wa manane. Katika hali hii ya mganganyiko, Mahakama ya Katiba imeamua kuchua hatu kwa taasisi husika.kugonga ngumu.

Hii ni dhoruba kali ya kisiasa inayoshuhudiwa kwa sasa nchini Gabon. Uamuzi wa Mahakama ya Katiba umesitisha shughuli za bunge na serikali. Bunge limevunjwa. Wakati huo huo, Seneti imeteuliwa kufanya shughuli za bunge kwa muda mfupi.

Kwa mshangao mkubwa, Marie-Madeleine Mborantsuo, Mkuu wa Mahakama ya Katiba, amechukua hatua dhidi ya taasisi hizi mbili akisema: "Mamlaka ya Bunge inasitishwa kufuatia uamuzi huu, ikiwa ni pamoja na shughuli za spika wa Bunge kwa taasisi hiyo. Ili kuhakikisha kazi nzuri ya mamlaka ya umma inaendelea vizuri, mamlaka ya bunge itawakilishwa na bunge la Seneti. "

Ni vigumu kwa wabunge kuendelea kushiriki vikao wakati ambapo umekwisha tangu miaka miwili iliyopita, Mahakama ya Katiba imeeleza.

Mahakama pia imeamua kuichukulia vikwazo serikali kwa kushindwa kuandaa uchaguzi wa wabunge. Serikali inmetakiwa kujiuzulu. Rais wa Jamhuri ametakiwa kuteua serikali ya mpito ambayo itakua na kai ya kuandaa uchaguzi wa wabunge.

Serikali, baada ya uchaguzi wa wabunge, pia italazimika kujiuzulu. Wakati huo huo, kutokana na kutokuepo kwa Bunge, serikali haitotakiwa kwenda mbele ya bunge la Senate kujibu maswali ambayo ingelijibu bunge . Serikali itasimama moja kwa moja mbele ya rais wa Jamhuri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.