rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Cameroon

Imechapishwa • Imehaririwa

Kanisa Katoliki latakiwa kuingilia mzozo wa Cameroon

media
Machafuko yamekua yakiendelea katika maeneo ya wazungmza Kiingereza, Cameroon.

Shirika la kimataifa la utatuzi wa mizozo la international Crisis group, limependekeza kuwa kanisa katoliki liingilie kati mzozo wa Cameroun unaendelea kukuwa kila uchao baina ya upande unaozungumza lugha ya kifaransa na ule unaozungumza Kiingereza.


Tangu kipindi kadhaa, kumeshuhudiwa mpasuko baina ya pande hizo mbili nchini huku upande unaozungumza kingereza ukidai mjitengo na kuomba uhuru wa kujitawala.

International Crisis Group inaona kuwa licha ya kanisa Katoliki kugawanyika, bado lina nafasi ya kuzileta pande zote mbili kwenye meza ya mazungumzo, kwa mujibu wa afisa wa International Crisis Group, Ansede Marie Ungu.

Asilimia 30 ya wananchi wa Cameroun ni Wakatoliki.

Maeneo ya kaskazini magharibi na kusini magharibi mwa Cameroon ni ya wakazi wanaozungumza lugha ya Kiingereza na wanaunda asilimia 20 ya wakazi wote wa nchi hiyo.

Mwaka mmoja uliopita maeneo hayo yamekumbwa na mapigano mengi ya ndani na kusababisha mgogoro mkubwa wa kijamii na kisiasa.

Takwimu zinaonesha kuwa, tangu ulipomalizika mwaka 2017 hadi hivi sasa, askari zaidi ya 28 wa serikali wameuawa katika mashambulizi ya watu wanaotaka kujitenga na kujitangazia nchi yao huko kusini magharibi mwa Cameroon.