Pata taarifa kuu
CAR-USALAMA

Rais Touadera ataka waasi kujiunga katika mchakato wa amani

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadera ametoa wito kwa makundi ya waasi kuweka silaha chini katika juhudi za kuhimiza amani nchini humo.

Wanajeshi wa kulinda amani kutoka Ureno wakiendesha chambulizi dhidi ya kundi la wanamgambo katika kata ya PK5,wanakoishi Waislamu wengi, Aprili 8, 2018.
Wanajeshi wa kulinda amani kutoka Ureno wakiendesha chambulizi dhidi ya kundi la wanamgambo katika kata ya PK5,wanakoishi Waislamu wengi, Aprili 8, 2018. FLORENT VERGNES / AFP
Matangazo ya kibiashara

Touadera ameuambia Umoja wa Mataifa kuwa, amewaagiza maafisa wa usalama kuja na mbinu za kuwahimiza waasi hao kuacha vita na kuwarudisha kwenye jamii.

Wito huu unakuja wakati huu makundi yenye silaha yakiendelea kuwa tishio kubwa kwa usalama wa nchi hiyo na hivi karibuni kulipotiwa kwa makabiliano kati yao na wanajeshi wa kulinda amani.

Machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya kati yamesababisha vifo vya watu wengi na wengine wengi kulazimika kuyahama makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.