Pata taarifa kuu
DRC-AFYA

Madaktari wagoma DRC

Madaktari nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaendelea na mgomo wao walioanza siku ya Jumatatu kwa wito wa chama chao kikuu. Madaktari nchini DR Congo wanaomba serikali kuboresha mishahara yao, huku wakiishutumu kutoheshimu makubaliano walioafikiana mwaka jana kuhusu madai yao.

Magari ya wagonjwa katika hospitali ya Cinquantenaire, DRC, Machi 2014.
Magari ya wagonjwa katika hospitali ya Cinquantenaire, DRC, Machi 2014. Junior D. Kannah / AFP
Matangazo ya kibiashara

Madaktari wanadai kupewa mshahara mzuri, malipo ya kazi zao za ziada, kutambuliwa kwa vyeo vyao na ufumbuzi kwa madaktari mia moja waliyofukuzwa kinyume cha sheria mwaka 2016 kwa mujibu wa madaktari hao, na ambao hufanya kazi tangu wakati huo bila malipo.

Jambo muhimu zaidi, madaktari wanalalamikia makubaliano ya hivi karibuni yaliyosainiwa mnamo Septemba 2017 na yangelipaswa kutatua masuala yote hayo yanayozua utata. Kwa mujibu wa madaktari makubaliano hayo hayajawahi kutekelezwa.

Wagonjwa wameomba madaktari kusitisha mgomo huo wakisem akuwa unawaathiri pakubwa, huku wakiomba serikali kutafutia ufumbuzi madai ya madaktari.

Mwishoni mwa wiki hiliyopita, serikali ilitoa mapendekezo kwa madaktari wanaogoma.Serikali inabaini kwamba tayari imejibu madai ya madaktari, huku ikisema kazi kubwa kwa sasa iko upande wa chama kikuu cha madaktari, ambacho hakikuwasilisha mapendekzo hayo kwa wanachama wake. Kwa wakati huu, hakuna mkataba umefikia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.