Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Kivu Kaskazini yaendelea kukumbwa na visa vya utekaji nyara

Baada ya kuripotiwa visa vya utekaji nyara vya mara kwa mara jijini Goma, mkoani Kivu Kaskazini,wanasheria kwa ushirikiano na mashirika ya kiraia jijini humo wametoa wito kwa viongozi wa serikali nchini Congo pamoja na mashirika ya mawasiliano kujitahidi katika kupambana dhidi ya visa hivyo sugu mkoani humo.

Malori yakisubiri kusindikizwa na vikosi vya usalama kwa kuvuka Hifadhi ya wanyama ya Virunga, Kivu Kaskazini.
Malori yakisubiri kusindikizwa na vikosi vya usalama kwa kuvuka Hifadhi ya wanyama ya Virunga, Kivu Kaskazini. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja watu zaidi ya watatu wametekwa nyara katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Baadhi ya mateka walifanyiwa mateso na kuzitaka familia zao kulipa fidia ili waweze kuachiwa.

Wanasheria Kaskazini mwa mkoa huo wanasema wamechoshwa na visa hivyo na ukimya wa serikali. Wamewataka viongozi serikalini hasa vikosi vya usalama na ulinzi kujihusisha zaidi katika mapambano dhidi ya visa vya utekaji nyara ambayo vimekithiri mkoani humo.

Mashahidi wanasema makundi hayo ya wa wahalifu yamekua yakitumia nambari za mashirika ya mawasiliano kwa kulazimisha kulipwa fedha. Airtel Money ni miongoni mwa mashirika ambayo makundi hayo yamekua yakizitaka familia za mateka wanaoshikilia kuweka pesa ili waweze kuachiwa.

Baadhi ya familia ambazo zililazimika kutoa fedha hizo zimekua zikijizuia kueleza chochote kwa kile kilowasibu.

Viongozi tawala katika mkoa wa Kivu Kaskazini wamevitaka vikosi vya usalama na ulinzi kuwa makini na kuzidisha doria kwa minajili ya kupambana dhidi utekaji nyara.

“Wanaoteka nyara raïa jijini Goma sasa ni wengi, wanajeshi wetu tunaomba wajitahidi zaidi dhidi ya visa hivi. Nao raia wetu wawe makini, “ Meya wa jiji la Goma Muisaa Kense Timothee.

Wakati huo huo shirika linalotetea haki za binadamu nchini DR Congo La Voix de Sans Voix, limetoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kutathmini usalama wa wananchi wake, baada ya tukio la uvamizi mwishoni mwa juma katika kanisa moja jijini Kinshasa na kuwapora waumini na kumjeruhi Mwinjilisti Jean Jacques Muwawa.

Shirika hilo limeitaka serikali kuanzisha uchunguzi kubaini wahusika wa tukio hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.