rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Zimbabwe Jumuiya ya Madola Emmerson Mnangagwa Robert Mugabe

Imechapishwa • Imehaririwa

Zimbabwe  kushiriki mkutano wa Jumuiya ya Madola

media
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa (kulia), Januari 24, 2018 Davos, Uswisi. AFP

Zimbabwe itashiriki katika Mkutano wa viongozi wa nchi kutoka muungano wa Jumuiya ya Madola unaofanyika wiki hii jijini London nchini Uingereza.


Itakuwa mara ya kwanza kwa Zimbabwe kurejea katika mkutano huo baada ya kufungiwa mwaka 2003 kwa sababu ya wizi wa kura na ukiukwaji wa haki za binadamu chini ya uongozi wa aliyekuwa rais Robert Mugabe.

Zimbabwe haijaalikuwa kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola tangu nchi hiyo kuzuiliwa kwa vikao vyote vya jumuiya hiyo tangu mwaka 2003.

Jumuiya ya Kimataifa iliigomea Zimbabwe kufuatia matokeo yanayobishwa na uchaguzi wa rais, mnamo mwezi Machi mwaka 2002. Kadhalika Muungano wa Ulaya ulitangaza vikwazo dhidi ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa makisio ya wachunguzi wa kimataifa, wakati huo Mugabe alishinda kwa matumizi ya mabavu, vitisho dhidi ya upinzani na ulaghai katika uchaguzi.

Zimbabwe ilijiunga na Jumuiya ya Madola tangu mwaka 1980.

Tambua Jumuiya ya Madola

Jumuiya ya Madola (jina la Kiingereza ni Commonwealth of Nations) inaunganisha nchi mbalimbali hasa Uingereza na nchi zilizokuwa koloni zake.

Umoja huu umeanzishwa mwak 1926 kama "Jumuiya ya Kibritania" (British Commonwealth) na kupewa jina lake la sasa tangu 1949. Inafuatana na Dola la Kibritania au Dola la Kiingereza ambalo lilikuwa dola kubwa kabisa katika historia ya dunia lakini maeneo yake yalianza kuachana baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia kutokana na kudhoofishwa kwa Uingereza vitani na miendo ya kupigania uhuru katika nchi mbalimbali hasa Uhindi.

Leo zipatao asilimia 30 ya watu wote duniani, huishi katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola. Nchi za jumuiya hii wenye wakazi wengi ni hasa Uhindi, Pakistan, Bangladesh na Nigeria. Kuna pia nchi ndogo sana kama Tuvalu yenye wakazi 11,000 pekee.

Nchi kadhaa zilisimamishwa uanachama au kuondoka kwa hiari zao. Mfano Tanganyika na Zanzibar ziliungana kwa hiyo hazipo tena, lakini mpya ya Tanzania imekuwa nchi mwanachama. Vilevile Newfoundland iliondoka katika jumuiya baada ya kujiunga na Kanada kama jimbo.

Pakistan ilisimamishwa uanachama mara kadhaa kwa sababu serikali yake ilipinduliwa na wanajeshi walioanzisha serikali ya kijeshi, na baadaye ilirudishwa tena.

Zimbabwe ilisimamishwa uanachama baada ya uchaguzi bandia 2002 ikaamua kujiondoa kabisa mwaka 2003.

Jamhuri ya Ueire iliamua mwaka 1949 kuacha viungo vyote na Uingereza ikajitangaza kuwa jamhuri isiyokubali athira ya nje kama hali ya malkia wa Uingereza kuwa mkuuw a dola hivyo ikaondoka katika jumuiya.

Afrika Kusini ilijiondoa 1961 kwa sababu ya upinzani wa jumuiya dhidi ya sheria za utawala wa ubaguzi wa rangi (apartheid). Baadaye mwisho wa ubaguzi wa rangi nchi hii ilirudi katika jumuiya.

Fiji ilisimamishwa mara kadhaa baada ya uasi wa kijeshi uliopindua serikali.