rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Rwanda

Imechapishwa • Imehaririwa

DRC kukabidhi askari wawili kwa Rwanda

media
Wanajeshi wa Serikali ya DRC wakiwa mjini Goma kujiandaa kukabiliana na waasi wa M23. RFI

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limesema kuwa askari wa Rwanda waliokamatwa mwishoni mwa juma lililopita katika mkoa wa Kivu Kaskazini watakabidhiwa mamlaka husika ili waweze kurejeshwa nchini Rwanda.


Kwa mujibu wa BBC Afrique, askari wawili wa Rwanda walikamatwa na silaha na vifaa vya mawasiliano usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu karibu na uwanja wa ndege wa Goma mashariki mwa DRC.

Kwa mujibu wa Meja Guillaume Ndjike, mmoja wa wasemaji wa jeshi la DRC katika mkoa wa Kivu Kaskazini, askari wa Rwanda watakabidhiwa kwa tume ya mseto yenye dhamana ya kukagua mipaka kati ya nchi hizo mbili.

Taasisi hii itahusika na kukabidhi askari hawa kwa serikali ya Rwanda.

Meja Ndjike ameiomba Rwanda kutumia utaratibu huo wakati askari wake wanapokuwa kwenye ardhi ya Rwanda.

Kumekuwa na mvutano kwa miaka kadhaa kati ya Rwanda na DRC, ambayo inashutumu jirani yake kusaidia makundi ya watu wenye silaha nchini humo.

Mapigano kati ya majeshi ya nchi hizi mbili yalisababisha vifo vya askari sita wa DRC mnamo mwezi Februari mwaka huu.