rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Siasa Joseph Kabila

Imechapishwa • Imehaririwa

Wafadhili wa Kimataifa wakutana Geneva kutafuta fedha za kuisaidia DRC

media
Rais wa DRC Joseph Kabila REUTERS/Kenny Katombe

Mkutano wa wafadhili kuisaidia DRC unafanyika siku ya Ijumaa nchini Uswisi huku takwimu za Umoja wa Mataifa zikionesha kuwa watu Milioni 13 wanahitaji msaada huku thuluthi moja kati yao wakiwa  ni wakimbizi wa ndani wanahitaji msaada wa dharura wa kibinadamu mwaka huu.


Wafadhili hao wa Kimataifa wanatafuta Dola Bilioni 1.5 kuwasaidia watu hao wanaohitaji dawa, chakula na makaazi mazuri kwa lengo la kuwasaidia.

Uingereza inayoshiriki katika mkutano huo imesema itatoa Dolla Milioni 31 na hii baada ya ziara ya waziri wa Uingereza anayehusika na masuala ua ya Afrika Harriett Baldwin nchini humo na kusema hali ni ngumu.

Pamoja na kutoa ahadi hiyo, Uingereza inataka kufanyika kwa Uchaguzi utakaokuwa huru na haki ili kuondoa mkwamo wa kisiasa nchini humo ambao umekuwepo kwa muda mrefu.

Uchaguzi nchini DRC umeratibiwa kufanyika tarehe 23 mwezi Desemba.

Hata hivyo, serikali ya Kinshasa imesusia mkutano huo, yakiishtumu mashirika ya kiraia kwa kutoa takwimu za uongo na kulichafulia jina taifa hilo.

Juvenal Munubo mbunge wa upinzani wa chama cha UNC amesema ingekuwa vema kwa serikali ya DRC kwenda katika mkutano huo kwa sababu raia wake ndio wanaoumia.