Pata taarifa kuu
NIGERIA-UNICEF-WATOTO

UNICEF: Watoto zaidi ya 1,000 walitekwa nchini Nigeria tangu 2013

Kundi la la Boko Haram liliwateka nyara watoto zaidi ya 1,000 tangu 2013 kaskazini mwa Nigeria, shirika la Umoja wa Mataifa kwa watoto (UNICEF)  limesema katika ripoti iliyochapishwa sikiu ya Ijumaa wiki hii.

Baadhi ya wanafunzi Kaskazini mwa Nigeria ambao wamewahi kujipata mikononi mwa magaidi wa Boko Haram
Baadhi ya wanafunzi Kaskazini mwa Nigeria ambao wamewahi kujipata mikononi mwa magaidi wa Boko Haram REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

 

Ripoti hii inatolewa wakati maadhimisho ya miaka nne ya kutekwa nyara kwa wasichana 276 wa shule ya Chibok.

"Watoto wa kaskazini mwa Nigeria wanaendelea kulengwa na mashambulizi katika kiwango cha juu," amesema Mohammed Malick Fall, Mkurugenzi wa UNICEF nchini Nigeria amesema.

Hii ni mara ya kwanza UNICEF kuchapisha ripoti inayotoa inayotaja idadi, kulingana na taarifa zilizokusanywa kwa kila kesi, idadi ya watoto waliotekwa nyara na kundi hili la Boko Haram.

Lakini UNICEF inasema kuwa takwimu ya kweli inaweza kuwa kubwa zaidi.

Unicef imeongeza kwamba karibu walimu 2,300 wameuawa na shule zaidi ya 1,400 ziliharibiwa katika kipindi hicho.

Boko Haram, ilichukua silaha mwaka 2009. Mfumo wa elimu ni moja ya malengo yake makuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.