Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA

Wasiwasi watanda kuhusu hatima ya Marshal Khalifa Haftar

Watu wengi nchini Libya wanaendelea kujiuliza, huku uvumi ukiendelea kuzaga kuhusu hatima ya Marshal Khalifa Haftar, kiongozi wa kundi la waasi linaloshikilia mashariki mwa Libya. 

Marshal Khalifa Haftar, katika mkutano na waandishi wa habari karibu na Benghazi, Jumamosi, Mei 17, 2014 (picha ya zamani).
Marshal Khalifa Haftar, katika mkutano na waandishi wa habari karibu na Benghazi, Jumamosi, Mei 17, 2014 (picha ya zamani). REUTERS/Esam Omran Al-Fetori
Matangazo ya kibiashara

Marshal Khalifa Haftar amelazwa katika hospitali moja mjini Paris, nchini Ufaransa, kwa mujibu wa familia yake, ambayo imebaini kwamba hali yake ya afya iko imara.

Kwa mujibu wa mashahidi kiongozi huyo wa waasi alipelekwa hospitali nchini Jordan siku ya Jumapili, lakini kufuatia jinsi hali yake ilivyokua, ililazimika asafirishwe katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris.

Duru za kuaminika zimeiambia RFI kwamba Marshal Haftar yuko Paris katika hospitali ya kijeshi. Dru hizi pia zinasema kwamba anaendelea vizuri. Taarifa ambayo imethibitishwa na familia yake.

Taarifa ya kuzorota kwa hali ya afya ya Khalifa Haftar ilianza kuzungumzwa katika vyombo vya habari vya Libya tangu siku Jumatatu alasiri wiki hii. Taarifa hizi zinabaini kwamba Khalifa Haftar alilazwa katika hospitali moja nchini Jordani, kisha ililazimika asafirishwe nchini Ufaransa ambako hali yake ya afya imeendelea kuwa mbaya.

Marshal Haftar alionekana mara ya mwisho Machi 28.

Hakuna taarifa yoyote ya kuaminika kwa sasa kuhusu sababu za kulazwa hospitalini. Lakini kwa mujibu wa familia ya Haftar, askari huyu nasumbuliwa na kansa, na kwa miezi kadhaa, amekua anaenda kwa nchini Jordan kwa matibabu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.