Pata taarifa kuu
MALI-UN-USALAMA

Mali yakabiliwa na shinikizo kutoka Umoja wa Mataifa

Mali imeendelea kujikuta ikikabiliwa na shinikizo kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kutokana na kushindwa kutekeleza ahadi zake kuhusu utekelezaji wa mkataba wa amani, Ufaransa na washirika wake wamesema kwamba wanataka kutambua wale wanaohusika na kutotekelezwa kwa mkataba huo.

Kambi ya kikosi cha walinda amani wa Umoja wa mataifa nchini Mali (Minusma) huko Gao, Mali.
Kambi ya kikosi cha walinda amani wa Umoja wa mataifa nchini Mali (Minusma) huko Gao, Mali. RFI/Olivier Fourt
Matangazo ya kibiashara

Wadau wote wa makubaliano ya amani ambao wana uhusiano na makundi ya kigaidi au wafanyabiashara haramu wanalengwa na wanaweza kujikuta kwenye orodha ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa.

Mwishoni mwa mwezi Januari, Ufaransa ilikaribisha kusainiwa kwa mkataba wa amani [Januari 19] kwa ajili ya utekelezaji wa makubaliano ya amani lakini ilionya kuwa ikiwa kutakua na ucheleweshaji, vikwazo kadhaa vinaweza kuchukuliwa.

Ni wazi kwamba "kuchelewa kwa utekelezaji wa mkataba huo kumesababisha athari kubwa". "Hatuna muda wa kusubiri," amesema balozi wa Ufaransa François Delattre ambaye alipata uungwaji mkono kutoka Uingereza, Marekani, Uholanzi, Ethiopia na Côte d'Ivoire, ambazo zimetaka majina ya wahusika yatajwe.

Serikali ya Mali na kundi la waasi la Azawad wananyooshewa kidole cha lawama kuhusika kwa njia moja ama nyingine kwa kushindwa kutekelezwa kwa mkataba wa amani nchini Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.