Pata taarifa kuu
ALGERIA. AJALI-USALAMA

Watu 257 wapoteza maisha katika ajali ya ndege ya kijeshi Algeria

Ndege ya kijeshi ya usafiri ya Algeria ilianguka mara tu baada ya kuondoka kutoka uwanja wa ndege wa kijeshi wa Boufarik, kilomita 30 kusini mwa Algiers Jumatano wiki hii. Watu 257 wamepoteza maisha katika ajali ya ndege hii, kulingana na ripoti ya kwanza rasmi iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi.

Ndege ya kijeshi ya Algeria ilianguka karibu na mji mkuu wa Algeria, Algiers, Aprili 11, 2017.
Ndege ya kijeshi ya Algeria ilianguka karibu na mji mkuu wa Algeria, Algiers, Aprili 11, 2017. REUTERS/Ramzi Boudina
Matangazo ya kibiashara

Ndege hii aina ya Iliouchine IL-76 ilianguka katika shamba moja karibu na uwanja wa ndege wa kijeshi wa Boufarik. Miongoni mwa waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni askari na familia zao. Abiria 247 na wafanyakazi kumi wa ndege hiyo wote wameangamia katika ajali hiyo.

Ndege hiyo ilianguka katika "sehemu ya kilimo" muda mfupi baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Boufarik huko Blida, kusini mwa Algiers.

Ndege hiyo ilikua ikielekea uwanja wa ndege wa kijeshi wa Tindouf, kwenye mpaka na Sahara Magharibi. Vyanzo vya Usalama, vilivyonukuliwa na gazeti la kila siku la Ennahar, vinabaini kwamba wajumbe 26 wa Polisario walikuwa katika ndege hiyo.

Mamlaka inajaribu kutafuta mabaki ya waliouawa. Picha kutoka eneo hilo zinaonyesha moshi ukifuka kutoka kwa vifusi vya mabaki ya ndege hiyo.

Naibu waziri wa Ulinzi, pia Mkuu wa majeshi ya Algeria, Jenerali Ahmed Gaid Salaha amezuru eneo la ajali.

Tume ya uchunguzi imeundwa ili kujua sababu ya ajali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.