Pata taarifa kuu
NIGER-HAKI

Familia ya rais wa zamani Baré Maïnassara: Tunataka kujua ukweli

Familia ya rais wa zamani wa Niger Ibrahim Baré Maïnassara, aliyeuawa tarehe 9 Aprili 1999 katika kambi ya kijeshi na askari wa kikosi chake cha ulinzi, bado wanaomba kujua ukweli kuhusu kifo cha rais huyo.

Rais wa zamani wa Nigeria Ibrahim Baré Maïnassara, ambaye aliuawa mnamo mwezi Aprili 1999, hapo alikua katika maombi baada ya uchaguzi wake Julai 7, 1996.
Rais wa zamani wa Nigeria Ibrahim Baré Maïnassara, ambaye aliuawa mnamo mwezi Aprili 1999, hapo alikua katika maombi baada ya uchaguzi wake Julai 7, 1996. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Miaka kumi na tisa baada ya kifo cha rais Ibrahim Bare Mainassar, familia yake bado inasubiri kujua waliohusika na mauaji hayo.

Mnamo mwezi Oktoba 2015, Mahakama ya ECOWAS ilitoa uamuzi kwamba "haki kwa maisha ya rais Ibrahim Baré Maïnassara ilivunjwa".

Mahakama hiyo iliomba serikali ya Niger kulipa fidia kwa familia ya kiongozi huyo wa zamani. Fidi hiyo tayari imetolewa. Lakini hatua moja ya hukumu haijatekelezwa hadi sasa, ambayo ni haki kwa maisha ya kiongozi huyo.

Mwanasheria wa familia, Abdouramane Chaibou, akihojiwa na RFI amesema.kama familia itakua bado haijajua waliohusika na kifo cha rais Ibrahim Bare Mainassara haiwezi kuwa na amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.