Pata taarifa kuu
MAREKANI-SAHEL-USALAMA

Zoezi la kijeshi la Flintlock 2018 kuzinduliwa Niger

Mpango wa kimataifa unaojulikana kama Flintlock unaoongozwa na Marekani unalenga kuimarisha uwezo wa kijeshi wa majeshi ya eneo la Sahel katika mapigano yao dhidi ya makundi ya kijihadi. Kila mwaka, mazoezi ya kijeshi ya pamoja yanafanyika.

Askari wa Nigeria wakipiga doria kati ya Agadez na Arlit.
Askari wa Nigeria wakipiga doria kati ya Agadez na Arlit. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mwaka huu wa 2018, mazoezi haya yatafanyika katika kambi ya jeshi la Marekani ya Agadez, nchini Niger, na yatazinduliwa Jumatatu hii Aprili 9.

Nchi nane za eneo la Sahel, ikiwa ni pamoja na wanachama wa G5 Sahel - Mali, Niger, Mauritania, Chad na Burkina Faso zitashiriki katika mazoezi hayo.

Hata kama Marekani imejiweka kando na mradi wa G5 Sahel uliopendekezwa na Ufaransa, imeendelea kutoa msaada wake katika uwanja wa vita.

Mwaka jana, nchi tatu pekee za eneo la Sahel zilishiriki katika mazoezi ya kimataifa yajulikanayo kama Flintlock. Mnamo mwaka huu wa 2018, nchi zinazounda eneo la Sahel zitakuwapo na nchi 12 za Magharibi ambazo ni washirika. Lengo ni kuimarisha uwezo wa majeshi ya eneo la Sahel pamoja na hatua zao za pamoja.

Marekani iliahidi kutoa Dola milioni 60 kwa kikosi cha G5 Sahel. Washington hata hivyo ilikumbusha kwamba misaada yake itatolea kama kwa kila nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.