rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Mauaji Dini

Imechapishwa • Imehaririwa

Waasi wa Mai Mai wamuua Padri Mashariki mwa DRC

media
Kikosi cha askari wa DRC (FARDC) wanaoendelea kupambana dhidi ya makaundi ya waasi mashariki mwa DRC. REUTERS/Kenny Katombe

Kasisi wa kanisa katoliki ameuawa kwa kupigwa risasi na waasi wa kundi la Mai Mai Nyatura Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo, kwa mujibu wa yanzo vya usalama.


Mauaji na visa vya utekaji nyara dhidi ya viongozi wa kanisa Katoliki vinaendelea kushuhudiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, hasa mashariki mwa nchi hiyo.

Vyanzo hivyo vimeongeza kuwa Padri √Čtienne Nsengiyumva aliuawa wakati wakati wa sherehe za ibada ya ubatizo wa wakristo wapya na wanandoa wapya.

Mashahidi wanasema mtu mwenye silaha aliingia kanisani na kumpiga risasi kasisi huyo.

Hii si mara ya kwanza kutokea kwa vitendo viovu dhidi ya viongozi wa kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katika kipindi kisichozidi wiki mbili Padri Havugimana Ngango Célestin alithibitishwa kutekwa nyara na waasi wasiojulikana katika maeneo ya Kihondo wilayani Ruchuru, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Padri Ngango alitekwa nyara na waasi wasio julikana akiwa kwenye gari lake kwenye barabara inayoelekea Kihondo katika eneo la Nyarukwangara ambako alisherehekea pasaka.

Mwanzoni mwa mwaka huu Padri mmoja alitekwa nyara na kundi la waasi ambalo halikujulikana.

Wanaharakati wa haki za binadamu wanaomba serikali ya DRC kufanya kazi yake ya kulinda raia ipasavyo.