Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Nigeria na Boko Haram wafanya mazungumzo ya chini kwa chini

Wakati ambapo machafuko kaskazini mashariki mwa Nigeria yaligharimu maisha ya watu 20 na zaidi ya 80 kujeruhiwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika mashambulizi ya kujitoa mhanga karibu na mji wa Maiduguri, serikali imetangaza kuwepo kwa mazungumzo ya amani na kundi la Boko Haram.

Vifusi vya nyumba katika mji wa Bama, kaskazini-mashariki mwa Nigeria baada ya mashambulizi yaliyotekelezwa na Boko Haram, Februari mwaka 2014.
Vifusi vya nyumba katika mji wa Bama, kaskazini-mashariki mwa Nigeria baada ya mashambulizi yaliyotekelezwa na Boko Haram, Februari mwaka 2014. AFP PHOTO / STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo ambayo yalikua yakifanyika kwa siri, yalianza miezi kadhaa iliyopita ili kupata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro ambao umeendelea kuathiri eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo kwa miaka kumi sasa.

Serikali ya Nigeria ilisubiri kuachiliwa huru kwa wasichana waliokolewa kutoka Dapchi ili waweze kuanzisha mazungumzo na kundi la Boko Haram. Rais wa nchi hiyo Muhammadu Buhari, Waziri wa Habari na Mkuu wa Idara ya ujasusi nchini wameamua kutangaza kuwepo kwa mazungumzo ya amani na Boko Haram. Wanajaili "uwezekano wa kusitishwa kwa moja kwa moja mapigano" na "uwezekano wa kutoa msamaha kwa wapiganaji wa kundi la Boko Haram". Mpango huu unaotakiwa na wengi nchini Nigeria unaonekana kukwama kutokana na migawanyiko ya ndani katika kundi la Boko Haram.

Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama, mazungumzo haya yanafanyika kati ya serikali na kundila Boko Haram linaloongozwa na Abu Musab al-Barnawi. Kundi linaloongozwa na Abubakar Shekau, limefutilia mbali mazungumzo yoyote na serikali.

Hii si mara ya kwanza kwamba Abuja atangaza ufunguzi wa majadiliano. Mwaka 2014, Rais wa zamani Goodluck Jonathan hata alidai kuwa amefikia makubaliano na wapiganaji, lakini mapigano yalianza tena.

Tangazo hili, linakujaikisalia mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa urais, na suala la usalama katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria ni mada nyeti. Muhammadu Buhari ambaye alichaguliwa mnamo mwaka 2015 juu ya kuleta amani katika eneo hilo linalodhibitiwa na Boko Haram, alikosolewa baada ya vurugu za hivi karibuni na utekaji nyara wa wasichana katika mji wa Dapchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.