Pata taarifa kuu
CAR-UN-USALAMA

Askari wa Minusca kutoka Misri auawa Gambo

Askari mmoja wa kikosi cha kimataifa cha kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya kati kutoka Misri aliuawa siku ya Jumapili usiku katika mji wa Gambo.

Askari wa kikosi cha Umoja wa Mataifa kutoka Pakistani akitoa ulinzi katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kaga-Bandoro mnamo Oktoba 19, 2016, Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Askari wa kikosi cha Umoja wa Mataifa kutoka Pakistani akitoa ulinzi katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kaga-Bandoro mnamo Oktoba 19, 2016, Jamhuri ya Afrika ya Kati. EDOUARD DROPSY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi dhidi ya askari wa kikosi cha Umoja wa Mataifa mnchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yanaendelea kushuhudiwa nchini humo.

Askari huyo aliuawa baada ya msafara wao kushambuliwa na kundi la watu wenye silaha.

Katika shambulizi hilo askari wengine watatu wa kikosi cha Minusca walijeruhiwa.

Wakati huo huo askari wa kikosi cha Umoja wa Mataifa waliwaua wapiganaji 5 na wengine kadhaa walikamatwa, kwa mujibu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Minusca, ambao umeshtumu baadhi ya askari wa serikali wenye uhusiano na makundi watu wenye silaha.

Tangu kudhibitiwa kwa mji wa Bangassou na kukamatwa kwa wanamgambo kadhaa miezi sita iliyopita, barabara hiyo ya kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati inayoelekea kwenye mpaka na DRC, ambayo inaunganisha Bangassou na Bambari, imekuwa moja ya maeneo hatari zaidi nchini humo.

Vurugu zimekua zikitokea mara kwa mara katika maeneo hayo. Wakati mwingine, mapiganoyamekua yakitokea kati ya wanamgambo na mahasimu wao hasa kundi la UPC, lenyre watu wengi kutoka jamii ya Peul. Lakini zaidi ya yote, mauaji ya raia, kama katika mji wa Pombolo mwezi uliopita; Pombolo ambakomsafara wa kikosi cha askari wa Umoja wa Mataifa Minusca walipambana na wanamgamo hao wenye silaha siku ya Jumapili. Minusca inachukuliwa na makundi haya ya wanamgambo "makundi ya kujihami kama maadui.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.