Pata taarifa kuu
MAREKANI-SOMALIA-AL SHABAB-USALAMA

Mashambulizi ya Marekani yaua wapiganaji watatu wa Al Shabab

Wapiganaji watatu wa Al Shabab wameuawa katika mashambulizi ya anga ya jeshi la Marekani, uongozi wa jeshi la Marekani umetangaza leo Ijumaa.

Uharibifu unaoendelea kufanywa na kundi la Al Shabab nchini Somalia.
Uharibifu unaoendelea kufanywa na kundi la Al Shabab nchini Somalia. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo yalitekelezwa kwa ushirikiano na majeshi ya Somalia karibu na mji wa Jilib, karibu kilomita 370 kusini magharibi mwa Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, jeshi la Marekani limesema katika taarifa yake.

Washington imeongeza shughuli zake za kijeshi nchini somalia, wakati ambapo Al Shabab, kundi lenye mafungamano na Al-Qaeda,linajaribu kupindua serikali inayoungwa mokono na nchi za Magharibi na kuiweka chini ya sheria za Kiislamu.

Kundi la A Shabab ilitimuliwa katika mji wa Mogadishu mnamo mwaka 2011 na kupoteza udhibiti wa vituo vingi vya miji ya Somalia. Lakini bado lipo katika sehemu nyingine za nchi na lina uwezo wa kufanya mashambulizi mabaya.

Al Shabab mara kwa mara inaendesha mashambulizi yake dhidi ya jeshi na raia.

Leo Ijumaa, askari mmoja aliuawa katika mji wa Mogadishu wakati wa shambulizi dhidi ya kituo cha ukaguzi. Shambulizi hilo lilitekelezwa na mwanamgambo wa Kiislamu.

Wakati huo huo mlipuko wa gari iliyotegwa bomu ambao utokea katika eneo hilo umewajeruhi askari wengine.

Kundi la Al Shabab limedai kuhusika na mashambulizi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.