rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afrika Kusini Jacob Zuma

Imechapishwa • Imehaririwa

Kesi ya Jacob Zuma yaahirishwa hadi Juni 8

media
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati wa ufunguzi wa kesi yake pamoja na mwakilishi wa Thales Christine Guerrier huko Durban tarehe 6 Aprili 2018. Nic Bothma/Pool via Reuters

Kesi ya aliye kuwa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma imeahirishwa hadi Juni 8. Jacob Zuma aliripoti katika mahakama ya Durban leo Asubuhi ili kujibu mashtaka ya rushwa, udanganyifu na kujitajirisha kinyume cha sheria.


Kesi hii imetarajiwa kusikilizwa kwa mara ya kwanza na inahusu biashara ya zamani ya mauzo ya silaha tangu miaka ya 1990.

Kesi hii ilidumu dakika kumi na mbili nakisha kuahirishwa. Jacob Zuma anashutumiwa kupokea rushwa kutoka kwa Thomson CSF - jina la zamani la kampuni ya Thales - katika mpango wa mkataba wa mauzo ya silaha wenye thamani ya karibu euro bilioni 4 ulioafikiwa mnamo mwaka 1999.

Wakati huo, Jacob Zuma alikua makamu wa rais wa nchi ya Afrika Kusini. Anashutumiwa kuwa alipokea jumla ya euro milioni 50 kutoka kampuni ya Ufaransa ya Thales. Kwa upande mwingine, aliahidi kupatishia zabuni kampuni hiyo ya Thales.

Kwa jumla, Afrika Kusini iliamua kutumia zaidi ya dola bilioni 10 kurejelea upya silaha zake. Silaha ambazo nchi hiyo haikuweza kuzihitaji wakati huo na ambazo hazitumiwi leo. Lakini sababu kuu ni kwamba zaidi ya dola milioni 300 (hongo) zililipwa wakati wa mikataba hii.

Andrew Feinstein, Mbunge wa chama cha ANC mwaka 1999 na mwanachama wa kamati ya bunge inayochunguza kesi hii amesema wana ushahidi tosha kuwa Jacob Zuma alipokea hongo kutoka kwa kampuni ya Thales.

Fedha hizo zilitumiwa kwa njia ya mpatanishi, Shabir Sheik, mshauri wa masuala ya kifedha wa Jacob Zuma. Ushahidi upo, ikiwa ni pamoja na faksi iliyotumwa na Alain Têtard, mkurugenzi wa kampuni ya Thales nchini Afrika Kusini, akihakikisha kuwa fedha zitawekwa katika akaunti iliyotolewa, kwa tarehe waliokubaliana kwa kazi alioahidi Jacob Zuma kwa kampuni hiyo.

Mnamo mwaka wa 2005, wawili hao walishutumiwa kwa kosa la rushwa, lakini Shabir Sheik alihukumiwa miaka 15 jela. Mashtaka dhidi ya Jacob Zuma yalifutwa mara kadhaa. Hasa katika usiku wa uchaguzi wake kama rais Afrika Kusini kwa makosa ya kiutaratibu.