Pata taarifa kuu
Sierra Leone-SIASA

Julius Maada Bio atangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais Sierra Leone

Kiongozi wa upinzani nchini Sierra Leone Julius Maada Bio, ametangazwa na tume huru ya uchaguzi nchini humo kuwa mshindi wa duru ya pili ya uchaguzi uliofanyika March 31.

Afisa wa zamani wa jeshi, ambaye alikaa madarakani kwa muda mfupi baada ya jaribio la mapinduzi, Julius Maada Bio ameshinda uchaguzi wa urais tarehe 5 Aprili 2018.
Afisa wa zamani wa jeshi, ambaye alikaa madarakani kwa muda mfupi baada ya jaribio la mapinduzi, Julius Maada Bio ameshinda uchaguzi wa urais tarehe 5 Aprili 2018. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Maada Bio mwanajeshi wa zamani mwenye umri wa miaka 53 ametangazwa kushinda nafasi hiyo kwa asilimia 51.81 dhidi ya mgombea wa chama tawala Samura Kamara aliepata asilimia 48.19.

Hata hivyo mgombea wa chama tawala Samaura Kamara amesema atakata rufaa mahakamani kupinga matokeo hayo yaliotangzwa na tume huru ya uchaguzi ambayo amesema hayakuzingatia malalamiko yake kuhusu dosari zilizojitokeza huku akiwatolea wito wafuasi wake kusalia kuwa watulivu na wenye mshikamano.

Wakati huo huo, Kelele, vifijo na Nderemo vimesikika jana usiku wakati mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi Nec Mohmaed Conteh alipotangaza matokeo hayo ambapo wafuasi wa chama cha upinzani cha wananchi nchini Sierra Leone. SLPP.

Saa mbili baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Julius Maada Bio alikula kiapo pia na kukabidhiwa madaraka kutoka kwa mtangulizi wake Ernest Bai Koroma ambae alishinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2012 na ambae asingeliweza kujichagulisha kwa mara nyingine tena baada ya kumaliza mihula miwili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.