rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Israeli UNHCR

Imechapishwa • Imehaririwa

UNHCR: Tuna matumaini kuwa Israel itarejelea upya uamuzi wake

media
Mmoja wa wahamiaji kutoka Afrika katika mji wa Tel Aviv, Aprili 19, 2012. Mamlaka ya Israeli inakadiria kuwa karibu wahamiaji 350,000 kutoka Afrika wanaishi nchini humo. REUTERS/Nir Elias

Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) ana matumaini kuwa Israeli "itarejelea upya" uamuzi wake wa kufuta makubaliano kuhusu wahamiaji wa Afrika ambayo yalikuwa yamekamilika.


"Tunaendelea kuamini katika haja ya makubaliano ambayo yangelinufaisha Israeli, jumuiya ya kimataifa na watu wanaohitaji hifadhi," amesema William Spindler, msemaji wa UNHCR , akiongezea: "tunatarajia kwamba hivi karibuni Israeli itarejelea upya uamuzi wake" wa kufuta makubaliano haya.

Mkataba huu unawapa hifadhi ya ukimbizi zaidi ya wahamiaji 16,000 kutoka Sudan na Eritrea wanaoishi nchini Israeli katika nchi za Magharibi. Israeli ilikua imeahidi kutafutia ufumbuzi suala la wahamiaji wengine ambao wangelibaki nchini humo.

"Nimesikiliza kwa makini maoni mengi juu ya mkataba huu na, baada ya kujaribu kutafakari faida na hasara, nimeamua kufuta makubaliano hayo," amesema waziri mkuu wa Israel katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Chini ya shinikizo kutoka kwa chama chake cha Likud, Benjamin Netanyahu alikuwa tayari aliufuta siku moja kabla, saa chache baada ya kutangaza hatua yake.