rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Mafuriko yameua watu kumi na nane Iran (idara ya hali ya Dharura)

Morocco UN

Imechapishwa • Imehaririwa

Umoja wa Mataifa wafutilia mbali madai ya Morocco kuhusu waasi

media
Brahim Ghali, lkiongozi wa Front Polisario, akihojiwa na shirika la habari la AFP, Februari 3, 2017. STRINGER / RYAD KRAMDI / AFP

Umoja wa Mataifa umefutilia mbali madai ya Moroccokuwa waasi wa Polisario Front walipenya na kuingia katika eneo ambalo hautakiwi upande wowote kungia humo, ambapo Umoja wa Mataifa unachunguza usitishwaji mapigano.


Siku ya Jumapili Morocco ilionya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba wapiganaji wa polisario Front waliingia katika mji wa Mahbes, kaskazini-mashariki mwa Morocco, siku za hivi karibuni, kwa kukiuka makubaliano ya kijeshi yaliyotenga eneo hilo.

"Wapiganaji kadhaa wa Polisario Front waliingia katika eneo hilo,wakiwa katika magari ya kijeshi, na walijenga sehemu ya kujihifadhi kwa mahema, huku wakichimba shimo na wakijenga sehemu hizo wakitumia magunia yaliojaa mchanga," ameandika balozi wa Morocco kwenye Umoja wa Mataifa, Omar Hilale, katika barua ambayo shirika la habari la AFP lilipata nakala.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric, kwa upande wake, aliripoti kuwa tume ya Umoja wa Mataifa katika eneo la Sahara Magharibi (Minurso) "halikuona mtu yeyote anayebebelea silaha katika eneo la kaskazini mashariki".

"Minurso inaendelea kuchunguza hali hiyo kwa karibu," Bw Dujarric ameongeza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco, Nasser Bourita, ametishia kutoa jibu la haraka dhidi ya uchokozi huo, na vitendo viovu vya waasi wa Polisario Front wakisaadiwa na Algeria ili kubadilisha sheria ya eneo hilo,lililotengwa tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990 chini usimamizi wa Umoja wa Mataifa.