rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Israeli Wahamiaji UNHCR

Imechapishwa • Imehaririwa

Netanyahu afuta makubaliano na Umoja wa Mataifa juu ya wahamiaji

media
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahukatika mkutano na waandishi wa habari. REUTERS/Ronen Zvulun

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amefuta makubaliano na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) kuhusu kuhamisha katika nchi za magharibi maelfu ya Waafrika waliowasili nchini Israel kinyume cha sheria.


"Nimesikiliza kwa makini maoni mengi juu ya mkataba huu na, baada ya kujaribu kutafakari faida na hasara, nimeamua kufuta makubaliano hayo," amesema waziri mkuu wa Israel katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Chini ya shinikizo kutoka kwa chama chake cha Likud, Benjamin Netanyahu tayari alifuta makubaliano hayo siku moja kabla, saa chache baada ya kutangaza hatua yake.

Hatima ya wakimbizi wa Kiafrika 37,000 inawachanganya raia wa Israel. Baadhi walikua wakimshinikiza Benjamin Netanyahu kuwafukuza, huku wengine wakibaini kwamba hatua ya kuwafukuza itakuwa ni kupinga sheria inayounda taifa la Israel, kama makao ya Wayahudi waliokimbia mateso.

Chini ya masharti ya mkataba 16250, takriban wahamiaji 37,000 kutoka Afrika waliowasili nchini Israel kinyume cha sheria, wengi wakitokea hasa Eritrea na Sudan wanapaswa kupelekwa katika nchi za Magharibi na wengine, kuruhusiwa kubaki nchini Israeli.

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Jerusalem, Benjamin Netanyahu amekaribisha makubaliano na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR).