Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SIASA

Waziri Mkuu mpya wa Ethiopia atawazwa

Waziri Mkuu mpya wa Ethiopia Abiye Ahmed, ambaye aliahidi kutekeleza mageuzi ya kidemokrasia, ikiwa ni pamoja na kupunguza matatizo ya mvutano wa kikabila katika jimbo la Oromiya anakotoka, ameapishwa leo Jumatatu mbele ya bunge.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiye Ahmed (picha).
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiye Ahmed (picha). REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Ethiopia mtu kutoka kabila ya Oromo kuwa waziri mkuu nchini Ethiopia.

Wiki iliyopita muungano wa vyama vilivyo madarakani ulimteua Abiye Ahmed, afisa wa zamani wa ngazi ya juu katika jeshi la Ethiopia, mwenye umri wa miaka 42, kumrithi Hailemariam Desalegn, ambaye alijiuzulu ili kufungua njia ya mageuzi.

Mkoa wa Oromiya unaozunguka mji wa Addis Ababa unakabiliwa na machafuko tangu mwaka 2015. Machafuko hayo yamesababishwa kwa kiasi kikubwa na hisia ya kubaguliwa kwa watu wengi kutoka kabila la Oromo, ambayo ina karibu theluthi moja ya wakazi milioni 100 wa Ethiopia.

Chama cha Revolutionary Democratic Front (EPRDF) kipo madarakani tangu kuchukua uongozi baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Derg mwaka 1991. Machafuko katika jimbo la Oromiya yamekua ni tishio kubwa kwa kuendelea kusalia madarakani tangu wakati huo. EPRDF ni muungano unaojumuisha vyama kadhaa vya siasa, ikiwa ni pamoja na chama kinachoundwa na watu wengi kutoka kabila la Oromo.

Abiye ameapishwa katika sherehe iliyohudhuria na baadhi ya wanasiasa wa upinzani waliokuwa wamealikwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.