rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Nigeria Boko Haram

Imechapishwa • Imehaririwa

Watu 15 wauawa katika shambulio la Boko Haram Nigeria

media
Vikosi vya usalama vikipiga kambi karibu na eneo la shambulizi linalodaiwa kutekelezwa na Boko Harampembezoni mwa mji wa Maiduguri, Nigeria Aprili 2, 2018. REUTERS/Ahmed Kingimi

Shambulio linalodaiwa kutekelezwa na kundi la Boko Haram liliwaua watu wasiopungua15 na kuwajeruhi 68 jana Jumapili jioni katika mji wa Maiduguri kaskazini mashariki mwa Nigeria, Idara ya huduma za dharura imesema leo Jumatatu.


Washambuliaji, ambao waliopenya na kuingia katika maeneo ya Bille Shuwa na Alikaranti, maeneo mawili yalio pembezoni mwa mji karibu na kijiji cha Biwa, walirudishwa nyuma, vyanzo vya kijeshi vimesema. Milipuko kadhaa iliripotiwa wakati wa urushianaji risasi kati ya wapiganaji hao na maafisa wa usalama.

"Watu sitini na nane walijeruhiwa na watu 15 wasio na hatia waliuawa," amesema Bello Dambatta, Mkuu wa Idara ya huduma za dharura (Sema). Idadi ta vifo inaweza kuongezaka, kulingana na vyanzo vya kijeshi.

Serikali ya Nigeria ilitangaza wiki iliyopita kuwa mazungumzo na kundi la Boko Haram yalianza kwa lengo la kusitisha mapigano.