rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Israeli Wahamiaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Israel yafuta mpango wake wa kufukuza wahamiaji wa Afrika

media
Wahamiaji 150 wa Sudan kwenye uwanja wa ndege wa Ben Gourion karibu na Tel Aviv wakielekea Khartoum. AFP PHOTO / JACK GUEZ

Israeli imetangaza leo Jumatatu kwamba imefuta mpango wake uliozua utata wa kuwafukuza wahamiaji kutoka Afrika. Israel pia imetangaza kwamba imesaini makubaliano na Umoja wa Mataifa kuwahamisha baadhi ya wahamiaji hao katika nchi za Magharibi.


"Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya wakimbizi na Israel wamefikia makubaliano kuruhusu kuondoka kwa wahamiaji takriban16,250 wa Afrika kwenda nchi za Magharibi, huku serikali ya Israeli ikitakiwa kuwapa hifadhi ya ukimbizi wahamiaji wengine watakaosalia nchini humo" , taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu imesema.

Hivi karibuni mamia ya wahamiaji wa Afrika waliamua kufanya mgomo wa kususia chakula wakati ambapo serikali ya Israel ilikua ikiendesha operesheni ya kuwakamata wahamiaji kulingana na mpango wake tata na kuwataka kuchagua kuondoka nchini humo au kufungwa jela

Umoja wa Mataifa ulikua uliitaka Israel kuachana na mpango huo wa kuwafukuza maelfu ya wahamiaji kutoka Afrika.

Mpango huo ulikua unahusisha wahamiaji 38,000, hasa kutoka Eritrea na Sudan.